Kazi za wanawake

Kazi za wanawake mara nyingi huchukuliwa kama ni kazi zinazowahusu wanawake pekee, na huhusishwa na kazi hizo kutokana na jinsia ya kike katika historia. Mara nyingi huchukuliwa kama kazi isiyolipwa ambayo mama au mke hufanya nyumbani na kwenye familia. [1]

Kazi za wanawake kwa ujumla si za kulipwa au hulipwa kidogo ukifananisha na "kazi za wanaume" na haithaminiwi sana kama hizo. [2] Kazi nyingi za wanawake hazijajumuishwa katika takwimu rasmi za kazi za nyumbani, na kusababisha kazi nyingi ambazo wanawake hufanya kwa kawaida zisionekane. [3] Kwa mfano, katika sehemu kubwa ya karne ya 20, wanawake wanaofanya kazi katika shamba la familia, bila kujali ni kazi ngapi walizofanya, walihesabiwa katika sensa ya Marekani kama awana ajira, wakati wanaume wanaofanya kazi sawa au hata kidogo walihesabiwa kama wanaofanya kazi kama wakulima.

  1. Borck, Larissa (Septemba 2019). "'A woman's work is never done': women's working history in Europe". Europeana (CC BY-SA) (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-27. Iliwekwa mnamo 2019-09-27.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Seager, Joni (2018). The Women's Atlas. Oxford: Myriad Editions. ku. 123, 126.
  3. Seager, Joni (2018). The Women's Atlas. Oxford: Myriad Editions. ku. 125.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search